Rais Abbas awataka Hamas waachie mamlaka ya Gaza
23 Aprili 2025Rais Mahmoud Abbas, amelitolea mwito kundi la wanamgambo la Hamas kuyakabidhi mamlaka ya Ukanda wa Gaza kwa utawala wa mamlaka ya ndani ya Wapalestina, kuweka chini silaha na kulibadilisha kundi hilo kuwa chama cha kisiasa,pamoja na kuwachia huru mateka wanaowashikilia.
Rais Mahmoud Abbas ametowa mwito huo katika hotuba aliyoitowa wakati wa mkutano uliofanyika Ramallah leo, ambako anatarajiwa kumtangaza mrithi wake.Soma pia: Rais wa Mamlaka ya Palestina awataka Hamas kuachia mateka
Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi ya kujibu wasiwasi wa kimataifa kuhusiana na uwezo wa Mamlaka ya Wapalestina kwa eneo hilo katika kipindi hiki kigumu.Soma pia: Pendekezo la Trump kuichukuwa Gaza lakabiliwa na upinzani mkali
Kundi hilo halijatowa tamko lolote kuhusu matamshi ya Rais Mahmoud Abbas. Wakati huo huo, shambulio la Israel lililofanywa usiku wa kuamkia leo dhidi ya shule moja iliyogeuzwa makaazi ya kuhifadhi watu, limeuwa watu 23 kwenye Ukanda wa Gaza.