Rais Macron apinga kuhamishwa kwa nguvu Wapalestina gaza
7 Aprili 2025Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametoa mwito wa kusitishwa vita katika Ukanda wa Gaza huku pia akipinga vikali juu ya kuondolewa Wapalestina kwenye makaazi na ardhi yao.
''Ufaransa inaungana na Misri katika swala hili muhimu, na ninataka kusisitiza kwa uzito kwamba tunapinga vikali kwa umma kuondolewa kwa lazima kutoka kwenye makazi yao na kuchukuliwa kwa nguvu kwa Ukanda wa Gaza pamoja na Ukingo wa Magharibi. Hatua hiyo itakuwa ni ukiukaji wa sheria ya Kimataifa na kitisho kikubwa kwa kanda hiyo ikiwemo kwa Israel''
Ujumbe huo wa rais Macron ameutoa akiwa ziarani mjini Cairo leo Jumatatu alikokutana na rais AbdelFatah el Sisi na kuipongeza Misri kwa mpango wake kuhusu ujenzi mpya wa Gaza, aliosema unatoa mwelekeo wa kiuhalisia.Soma pia:Israel yaonya kuwa haitosita kushambulia mahali popote nchini Lebanon
Macron amesema anaunga mkono mpango huo ulioidhinishwa na Jumuiya ya nchi za Kiarabu na akasisitiza kwamba kundi la Hamas halipaswi kuwa na dhima ya uongozi Gaza wala kusababisha kitisho kwa Israel.