Rais Lula alaani tishio la Trump la kuongeza ushuru kwa 50%
18 Julai 2025Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil, amelaani tishio la Donald Trump la kutoza ushuru wa asilimia 50 kwa bidhaa za Brazil na kusema kuwa ni hatua isiyokubalika.
Lula ametoa matamshi hayo wakati wa hotuba yake kwa taifa ikiwa ni mfululizo wa majibizano ya mvutano kati ya viongozi hao, huku rais wa Marekani akianzisha mashambulizi makali dhidi ya serikali nchini Brazil.
Katika hotuba yake, kiongozi wa mrengo wa kushoto aliwakashifu wanasiasa wa Brazil ambao "wanaunga mkono" sera za Trump kama "wasaliti kwa nchi."
Mnamo Julai 9 Trump alitangaza nia yake ya kuongeza ushuru mkubwa kwa Brazil kama adhabu kwa kile alichokiita hujma dhidi ya mshirika wake wa siasa kali za mrengo wa kulia Jair Bolsonaro.
Ushuru wa bidhaa zote kutoka Brazili utaanza Agosti mosi ikiwa Brasil na Washington hazitafikia makubaliano.