Rais Horst Köhler wa Ujerumani asifu uhusiano kati ya nchi yake na Israel miaka 40 tangu ulipoanzishwa
12 Mei 2005Matangazo
Rais wa shirikisho Horst Köhler na kiongozi mwenzake wa Israel Mosche Katzav wamesifu urafiki uliodumu miaka 40 tangu uhusiano wa kibalozi ulipoanzishwa kati ya Ujerumani na Israel.“Nchi hizi mbili zimekua washirika na rafiki“ amesema rais Horst Köhler aliyeshadidia lakini miaka 40 ya uhusiano wa nchi hizi mbili,isiwe sababu ya kutulia. Rais wa shirikisho ametilia mkazo umuhimu wa kuimarishwa uhusiano huo kwa miongo kadhaa mengine ijayo.“Kusambaza kwa pamoja demokrasia na haki za binaadam ni jukumu la pamoja la Ujerumani na Israel“ amesema rais wa shirikisho Horst Köhler.