Rais George W. Bush ameishukuru Ujerumani kwa msaada wake kwa wahanga wa kimbunga Katrina
6 Septemba 2005Matangazo
Mataifa kadhaa yamejitolea kuwasaidia wahanga wa kimbunga Katrina nchini Marekani.Ujerumani imetuma meli iliyosheheni mafuta kusaidia kupunguza uhaba wa mafuta nchini Marekani.Na jeshi la shirikisho Bundeswehr linasaudia pia kusafirisha misaada.Serikali kuu ya Ujerumani imetuma ndege ya kijeshi Pensacola Florida ikisheheni tani 15 za misaada ya dharura.Rais George W. Bush amemtumia risala ya shukurani kansela Gerhard Schröder.