Mnangagwa atangaza kufuta ushuru kwa bidhaa za Marekani
6 Aprili 2025Amesema hatua hiyo inakusudia kuongeza uagizaji wa bidhaa za Marekani kuingia katika soko la Zimbabwe na kukuza usafirishaji wa bidhaa za nchi yake zinazopelekwa Marekani.
Ametoa tamko hilo siku kadhaa baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kutangaza kuzitoza ushuru wa asilimia 18 bidhaa zote zinazotoka Zimbabwe. Nchi hiyo imekuwa ikiilaumu Marekani kwa kuisababishia mkwamo wa uchumi kutokana na vikwazo ilivyoiwekea kwa zaidi ya miongo miwili.
Soma zaidi: Marekani yatangaza vikwazo dhidi ya rais wa Zimbabwe
Mwaka uliopita Washington ilimwekea vikwazo Rais Mnangagwa na viongozi waandamizi wa serikali yake kwa tuhuma za kukiuka haki za binadamu na ubadhirifu. Mwandishi habari mashuhuri nchini humo Hopewell Chin'ono amesema tamko la kiongozi huyo ni juhudi za kutaka vikwazo dhidi ya Zimbabwe viondolewe, huku akidai nchi hiyo haisafirishi bidhaa nyingi Marekani kiasi cha kutaka kumridhisha Trump.