Rais Macron atowa mwito vita visitishwe Ukanda wa Gaza
7 Aprili 2025Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametowa mwito wa kusitishwa vita katika Ukanda wa Gaza, akiwa ziarani nchini Misri ambako pia amesisitiza kuondolewa kwa vizuizi dhidi msaada wa kibinadamu unaopelekwa Gaza.
Macron amekutana na rais AbdelFattah el Sisi mjini Cairo leo Jumatatu na baadae na mfalme Abdulla wa pili wa Jordan, wote wakiwa ni washirika wa karibu wa nchi za Magharibi, na ambao pia wamekuwa wakitowa mwito wa kusitishwa vita Gaza.Ujerumani, Ufaransa na Uingereza zasema vita vya Gaza viishe
Israel ilianza tena kuwashambulia Hamas mwezi uliopita na kuzuia usafirishwaji wa chakula mafuta na msaada wa kibidamu kwa Wapalestina takriban milioni 2 wanaoishi Gaza, kama hatua ya kujaribu kulishinikiza kundi la Hamas kukubali masharti mapya ya makubaliano ya kusitisha vita.