MigogoroAmerika ya Kaskazini
Rais Donald Trump awataka Putin na Zelensky kukutana
22 Februari 2025Matangazo
Trump amewaambia waandishi wa habari katika Ikulu ya White House kuwa anadhani ni wakati sasa kwaVolodymyr Zelenskyyna Vladimir Putin kukutana ili mamilioni ya watu wasiendelee kuuawa.
Wito huo mpya wa Trump unafuatia maoni ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio jana Ijumaa, aliyesema mkutano unaoweza kuwakutanisha Trump na Putin utategemea hatua zilizopigwa katika kumaliza vita nchini Ukraine."
Kwa mujibu wa Rubio, Trump anataka kujua iwapo Urusi ina nia ya dhati ya kumaliza vita vya Ukraine, vilivyochochewa na uvamizi kamili wa Moscow miaka mitatu iliyopita.