UchumiSyria
Marekani yaiondolea rasmi Syria vikwazo
1 Julai 2025Matangazo
Trump aitangaza nia ya kuondoa vikwazo hivyo kama mwezi mmoja na nusu uliopita, wakati alipofanya ziara Mashariki ya Kati.
Msemaji wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt amesema kabla ya kusainiwa kwa amri hiyo kwamba, inalenga kukuza na kuunga mkono njia ambayo taifa hilo inatumia ya utulivu na amani.
Lakini vikwazo vya Marekani dhidi ya Rais wa zamani wa Syria Bashar al-Assad na washirika wake havitaondolewa imesema Ikulu ya White House, lakini pia vikwazo kwa wanaokiuka haki za binadamu, walanguzi wa dawa za kulevya na watu binafsi wanaohusishwa na silaha za kemikali.
Tangu kupinduliwa kwa Assad mnamo Disemba, uongozi mpya wa Syria umekuwa ukipambana kurejesha ushirika na jumuiya ya kimataifa na kutaka kuondolewa kwa vikwazo vyote.