Rais Donald Trump amuita Zelensky Dikteta
20 Februari 2025"Amekataa kufanya uchaguzi, hana umaarufu katika kura za maoni ya Waukraine wenyewe. Unawezaje kuendelea kuwa juu, huku kila mji umeharibiwa? Ni vigumu sana....kuna mtu anasema, hapana bado umaarufu wake uko juu. Tafadhali, niache.'' Alisema Trump
Kauli ya Trump ya kumshambulia Zelensky imetolewa siku moja baada ya kiongozi huyo wa Marekani, kudai kwamba Ukraine inapaswa kulaumiwa kuhusu uvamizi uliofanywa na Urusi mwaka 2022.
Soma pia:Trump amuita Zelensky "Dikteta ambaye hakuchaguliwa"
Rais Zelensky alikataa kwenda Riyadh kujadili na Urusi na Marekani kuhusu amani. Waziri wa Mambo ya Nje wa Ukraine Andrii Sybiha, badala yake amesema hakuna anayeweza kuifanya nchi hiyo kusalimu amri.
Mtazamo wa Trump umeleta wasiwasi miongoni mwa washirika wa Marekani barani Ulaya, kwamba mwelekeo wa kiongozi huyo wa kumaliza vita kati ya Urusi na Ukraine huenda ukawa na maslahi zaidi kwa Urusi.