Raia wa Kongo wakimbilia Burundi kusaka hifadhi
1 Aprili 2025Ni katika tarafa ya Rugombo mkoa wa Cibitoke eneo linalopakana na DRC kupitia mto Rusizi, kuliko fikiwa idadi kubwa ya wakimbizi, kutoka maeneo mbali mbali ya mashariki mwa Kongo. Kambi kadha zimeundwa katika tarafa hiyo ya Rugomba ikiwa ni pamoja na kwenye uwanja wa michezo wa hapo Rugombo, kwenye shule ya upili ya Ecofo Rugombo, na kwenye shule ya tarafa. Mkimbizi Fedha Ramadhan anasema alivuka mto Rusizi na kuingia Burundi baada ya mumewe na watoto kuuawa. Pia anasema amekimbia mikono mitupu bila ya kubeba chochote huko alikotoka.
"Tangu nimefika hapa sijapata kitu sufuria au hata kikombe cha kunywa maji. Nimekuja mikono mitupu vitu vilichuliwa na maji, mume wangu na watoto wangu wamekufa. Kuna msongamano mkubwa wa kutoa Msada hivyo sijapata kitu," alisema Fedha Ramadhan.
Machafuko yazuka tena Mashariki mwa Kongo
Serikali ya Burundi kupitia wizara ya mambo ya ndani, maendeleo ya jamii na usalama inayohusika na suala la wakimbizi imekuwa ikihamasisha mashirika ya kimataifa na kitaifa kuchangia katika kukabiliana na changamoto zinazo wakambili wakimbizi hao. Waziri husika Martin Niteretse anasema imeundwa tume ya kufuatilia kwa karibu swala la wakimbizi hao kutoka nchi jirani ya DRC.
"Katika dhamira ya kuwarahisishia maisha wakimbizi, ndugu zetu hao kutoka Congo, tume hiyo inalo jukumu la kuhakikisha wakimbizi hao wako katika hali salama, pili kuwapatia sehemu za kulala chakula na matibabu, Wakimbizi waloingia Burundi tangu mwanzoni mwa mwaka huu wa 2025, wanatakiwa kupelekwa katika kambi ya Musenyi iliyo Rutana kama inavyo agiza sheria ya kimataifa. Serikali ya Burundi inatowa wito wa kuwepo na mshikamano kitaifa na kimataifa ili kufaanikisha zoezi hilo la kuwapokea na kuwahudumia wakimbizi kutoka Congo," aliongeza kusema Waziri Niteretse.
Shirika la UNHCR lahitaji fedha zaidi kuwashughulikia wakimbizi wa Kongo
Shirika la Umoja wa Mataifa linalo husika na wakimbizi limekuwa likitembelea kambi hizo ili kufanya makadirio ya mahitaji ya wakimbi.
Brigite Mukanga Muakilishi wa UNHCR Burundi, akiambatana na wanabalozi wa Afrika Kusini na yule wa Tanzania anasema kunahitaji chakula, madawa, vyoo, na vifaa vya kueneza nishati ya umeme katika maeneo waliko piga kambi wakimbizi.
"Hapa Rugombo tumeshuhudia kuna wakimbizi elf 47, tunawasiliana na Unicef ili ziungwe shule za dharuza zitakazo wapokea watoto wakimbizi. Na kwenye hatua ya kwanza kabisa ni kukamilisha zowezi la kuwasajili wakimbizi ili wapelekwe Musenye mkoani Rutana," alisema muakilishi huyo wa UNHCR Burundi nchini Burundi Brigite Mukanga.
UN yasema inahitaji ufadhili zaidi kuwalisha wakimbizi wa DRC Burundi
Mashirika ya kitaifa, yale ya kidini na hata raia wa kawaida wa wamekuwa wakiwapelekea misaada wakimbizi hao. Dieudonne Nahimana anaye ongoza shirikiso la Mac linalo undwa na mashirika ya kidini aliwapelekea msaada wa unga wa ugali. Na kuwafariji wakimbizi hao akisema kuwa jirani ni ndugu, na kwamba japo msaada alioupeleka ni mdogo, umetoka moyoni.
Shirika la UNHCR limekwisha towa makadirio ya dola milioni 40 nukta 4 zinazo hitajika ili kukidhi mahitaji ya wakimbizi hao kutoka DRC walokimbilia Burundi.
Amida ISSA