MigogoroUlaya
Raia watatu wauawa Kherson kufuatia mashambulizi ya Ukraine
25 Januari 2025Matangazo
Hayo yameelezwa siku ya Jumamosi na Vladimir Saldo, Gavana wa eneo hilo aliyewekwa na utawala wa Moscow ambaye amesisitiza kuwa eneo hilo bado ni hatari kwa raia kutokana na uwepo wa mabomu ya kutegwa ardhini ambayo hayajalipuka.
Mbali na hayo, wizara ya Ulinzi ya Urusi imesema ilidungua droni 11 za Ukraine kwenye anga ya Bahari Nyeusi karibu na rasi ya Crimea huku droni tatu zikidunguliwa huko Belgorod. Ukraine pia imedai kuyazima mashambulizi kadhaa ya Urusi ikiwa ni pamoja na kudungua droni 46.