MigogoroMsumbiji
Raia wauawa katika mashambulizi mapya kaskazini mwa Msumbiji
18 Machi 2025Matangazo
Haya yamesemwa jana na wakazi wa eneo hilo.
Kulingana na wakazi hao, waasi walivamia kijiji kimoja cha wilaya ya Meluco katika mkoa wa Cabo Delgado mapema jana na kumuuwa mtu mmoja.
Mwanakijiji mmoja aliyezungumza na shirika la habari la AFP kwa sharti la kutotajwa jina, amesema waasi hao waliingia nyumbani kwa mtu huyo na kuchukuwa mbuzi wake, lakini alipokuwa anakaidi walimkata kichwa.
Soma pia:Chapo aahidi kuiunganisha Msumbiji
Wakazi hao wameongeza kuwa waasi hao, walivamia takribani nyumba 10, kuiba mali na baadaye kuziteketeza.
Baadhi za nyumba hizo zilikuwa za machifu wa eneo hilo.
Chanzo kimoja cha kijeshi pia kilithibitisha kuhusu shambulizi hilo na kusema liliwalazimisha wakazi kukimbilia maeneo ya karibu.