Watu wanne waumeuawa katika maandamano nchini Angola
29 Julai 2025Matangazo
Msemaji wa polisi nchini humo Mateus Rodrigues amesema waandamanaji walipora na kufanya uharibifu katika benki, maduka, mabasi na magari binafsi.
Makabiliano kati ya polisi na waandamanaji yameripotiwa katika tukio hilo. Vurugu hizo zimeendelea Jumanne kwenye maeneo kadhaa ya mji mkuu Luanda. Tangazo la kupandisha bei ya mafuta lilisababisha vyama vya waendesha magari ya abiria kuongeza nauli zao hadi asilimia 50 ambapo vilianzisha maandamano ya siku tatu ili kuipinga hatua hiyo. Takriban watu 500 wamekamatwa kutokana na vurugu hizo.