SiasaKorea Kusini
Raia wa Korea Kusini wamchagua rais mpya
3 Juni 2025Matangazo
Kura zote za maoni zimemuweka mbele mgombea wa kiliberali, Lee Jae-myung, huku utafiti wa karibuni uliofanywa na shirika la Gallup ukionyesha asilimia 49 ya washiriki wakimchukulia kama mgombea bora zaidi.
Kim Moon-soo wa chama cha kihafidhina cha People Power, PPP, alimfuatia Jae-myung kwa asilimia 35, kwenye utafiti huo.
Yoyote atakayeshinda kwenye uchaguzi huo atalazimika kuanza mara moja kushughulikia masuala kuanzia ya kiuchumi, kiwango cha uzazi na udhibiti wa mipango ya silaha inayozidi kuimarika ya Korea Kaskazini.