Raia 11 wa Alawite wauawa katika uvamizi wa kiusalama syria
25 Aprili 2025Kwa mujibu wa shirika hilo la Syrian Observatory for Human Rights,, miongoni mwa waliouawa ni mwanafunzi wa chuo kikuu, aliyeuawa wakati wa uvamizi huo uliofanywa na maafisa wa usalama pamoja na makundi washirika.
Mauaji hayo yametajwa kuwa ya kimadhehebu, yakilenga jamii ya Alawi ambayo ni moja ya makundi ya wachache nchini humo.
Save the Children: Watoto zaidi ya 400,000 nchini Syria hatarini kukabiliwa na utapiamlo
Aidha, shirika hilo limeeleza kuwa watu watatu waliouawa waliteswa kabla ya kuuawa, baada ya kuzuiliwa na vikosi vya usalama.
Ripoti hiyo inabainisha kuwa mkoa wa Homs umekuwa ukishuhudia ongezeko lavitendo vya mauaji, ukiukwaji wa haki za binadamu na ghasia zinazofanywa na vyombo vya usalama bila kuwajibishwa.
Je, serikali mpya ya Syria inaweza kujumuisha makundi yote?
Katika taarifa nyingine, shirika hilo limeongeza kuwa katika vurugu za mwezi uliopita pekee, vikosi vya usalama na washirika wao waliwaua zaidi ya raia 1,700 – wengi wao wakiwa ni kutoka jamii ya Alawi.