MigogoroMashariki ya Kati
Qatar: Mpango wa Israel unadhoofisha juhudi za amani Gaza
9 Agosti 2025Matangazo
Serikali ya Doha imesema uamuzi huo unaokosolewa vikali kimataifa, unadhoofisha juhudi za kufikiwa makubaliano ya kusitisha mapigano.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imesema katika taarifa yake kuwa mpango wa Israel wa "kuikalia kikamilifu Gaza" ni hatari na unaweza kuchochea kuzidi kuporomoka kwa hali ya kibinadamu ambayo tayari ni janga.
Kulingana na mpango uliopendekezwa na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na kuidhinishwa mara moja na Baraza la Usalama, Israel itaanzisha mashambulizi mapya ya kijeshi kote Gaza lakini haikuwa wazi kwenye mpango huo ulioidhinishwa ikiwa Israel itachukua udhibiti kamili wa Ukanda wa Gaza.