Qatar yapinga kauli kali ya Israel dhidi yake juu ya Gaza
4 Mei 2025Matangazo
Waziri Mkuu wa Israel benjamin Netanyahu amesema kwamba Qatar inapaswa kuacha undumilakuwili katika mazungumzo ya upatanishi. Ofisi ya waziri mkuu wa Israel imesema nchi hiyo inaitaka Qatar inayoshirikiana na nchi zingine katika kuzipatanisha Israel na wanamgambo wa Hamas, ichague kati ya upande wa ustaarabu au upande wa Hamas.
Soma pia: Qatar yahuzunishwa na mchakato wa mazungumzo kuhusu Gaza
Kwa upande wake wizara ya mambo ya nje ya Qatar kupitia msemaji wake Majed al-Ansari imesema kwenye mtandao wa kijamii wa X kwamba nchi hiyo inapinga kwa uthabiti, kauli za uchochezi na zilizopungukiwa viwango vikuu vya uwajibikaji wa kisiasa na kimaadili.