Qatar yahuzunishwa na mchakato wa mazungumzo kuhusu Gaza
21 Aprili 2025Matangazo
Katika mahojiano na shirika la habari la AFP, Mohammed Al-Khulaifi amesema wanakatishwa tamaa na ucheleweshaji na hata mchakato mzima wa mazungumzo hayo.
Kauli hiyo inatolewa ikiwa ni mwezi mmoja tangu Israel kuanzisha wimbi jipya la mashambulizi katika ardhi ya Palestina ambapo duru nyingine ya mazungumzo imemalizika bila kufikiwa makubaliano yoyote, licha ya upatanishi wa Qatar, Misri na Marekani.
Hayo yakijiri Israel imekuwa ikiendeleza mashambulizi yake huko Gaza na kusababisha vifo vya makumi ya watu.