Qatar: Serikali DRC na M23 wamepewa rasimu ya amani
18 Agosti 2025Afisa anayehusika na juhudi za upatanishi ametangaza "kuandaliwa na kusambazwa kwa rasimu ya makubaliano ya amani kwa pande zote mbili kama sehemu ya mchakato unaoendelea wa Doha", huku Doha ikitarajiwa kuwa mwenyeji wa "awamu muhimu ya mazungumzo" hivi karibuni. Amesema muda uliopangwa haukufikiwa, lakini "pande zote mbili zimejibu kwa njia chanya kwa mpatanishi na wameonyesha nia ya kuendelea na mazungumzo". Serikali ya Kongo na kundi la M23 walitia saini tamko la kanuni tarehe 19 Julai huko Qatar, wakilenga kusaini makubaliano ya amani ifikapo tarehe 18 Agosti.Tangu 2021, kundi la M23 limefanikiwa kuyateka maeneo makubwa kwa msaada wa Rwanda, na hali hiyo imechochea mgogoro mkubwa wa kibinadamu. Mapema mwaka huu, waliteka miji muhimu ya Goma na Bukavu, na kuanzisha tawala zao katika maeneo hayo.