MigogoroMashariki ya Kati
Qatar: Mazungumzo ya kusitisha vita Gaza yatahitaji muda
8 Julai 2025Matangazo
Msemaji wa Wizara hiyo Majed al-Ansari amesema majadiliano hayo yamejikita zaidi katika mfumo wa mazungumzo.
Wakati juhudi hizo za kuutatua mzozo wa Gaza zikiendelea, Waziri wa Usalama wa Taifa wa Israel Itamar Ben Gvir amemtaka Waziri wake Mkuu Benjamin Netanyahu aurejeshe nyumbani ujumbe unaofanya mazungumzo na kundi la Hamas nchini Qatar. Kupitia ukurasa wake wa X, Ben Gvir ametaka Gaza izingirwe kikamilifu, isambaratishwe kabisa na Wapalestina wahamie nje ya Ukanda wa Gaza.