Pyramids FC ya Misri yabeba ubingwa Afrika
2 Juni 2025Matangazo
Klabu ya kandanda ya Pyramids FC ya nchini Misri imeandika historia mpya usiku wa kuamkia leo baada ya kulitwaa taji la Ligi ya Mabingwa barani Afrika kwa mara yao ya kwanza baada ya kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
Magoli ya Pyramids yalitiwa kimiani na Fiston Mayele na Mohamed Chibi huku goli la kufuatia machozi la Mamelodi Sundowns likifungwa na Iqraam Rayners.
Katika mchezo wa fainali ya kwanza uliochezwa nchini Afrika Kusini timu hizo mbili zilitoka sare ya 1-1 na hivyo kuifanya Pyramids kushinda kwa jumla ya magoli 3-2.
Pyramids ni timu ya nne ya nchini Misri kubeba taji hilo baada ya Al Ahly, Zamalek na Ismailia.