SiasaUrusi
Putin: Urusi haitishwi na inao uwezo wa kukabiliana na NATO
19 Juni 2025Matangazo
Akizungumza na wahariri wa mashirika ya habari ya kimataifa kwenye mji wa kaskazini mwa Urusi wa St.Petersburg, Putin amelipongeza jeshi lake kwa mafanikio kwenye vita vyake na Ukraine na kusisitiza kuwa wamekuwa wakiboresha mifumo yao ya ulinzi.
Viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya kujihami ya NATO wanatarajiwa kujumuika katika mkutano wa kilele wiki ijayo mjini The Hague, Uholanzi, huku kukiwa na msukumo wa kuzitaka nchi hizo kuongeza matumizi yao ya ulinzi kufuatia uvamizi wa Urusi nchini Ukraine ambao umepelekea vita vilivyodumu kwa zaidi ya miaka mitatu.