MigogoroUlaya
Putin: Tunatarajia mazungumzo zaidi na Ukraine
1 Agosti 2025Matangazo
Putin amesema angependelea kuwepo amani ya kudumu na utulivu nchini Ukraine, lakini akasisitiza kuwa kwa sasa muelekeo wa vita unaonyesha mafanikio makubwa kwa Urusi.
Rais wa Marekani Donald Trump amelaani mashambulizi ya Urusi hapo jana mjini Kiev yaliyowaua watu 31 na kuwajeruhi wengine zaidi ya 150 huku akitishia kuiwekea vikwazo Moscow.
Nitajaribu kusitisha vita hivyo. Lakini nadhani kile ambacho Urusi inafanya ni cha kusikitisha. Warusi wengi wanakufa. Waukraine wanakufa. "Ndio, tutaweka vikwazo. Lakini sijui kama vikwazo vinamsumbua.”
Trump alitangaza kuiwekea Urusi vikwazo ikiwa kufikia Agosti 8, haitoonyesha dalili zozote za kusitisha mapigano huko Ukraine.