Putin na Xi wampongeza Lukashenko kwa kushinda Urais Belarus
27 Januari 2025Matangazo
Aidha Putin amesema uchaguzi wa jana Jumapili umeonyesha bila shaka kuwa kiongozi huyo anaungwa mkono na watu wa Belarus.
Umoja wa Ulaya na wapinzani walioko uhamishoni au magerezani wamekosoa vikali uchaguzi huo wakisema haukuwa huru na wa haki.
Lukashenko ameshinda muhula wa saba mfululizo madarakani na ameikuwa akiiongoza Belarus kwa mkono wa chuma tangu mwaka 1994.
Soma pia:Lukashenko arefusha utawala wake madarakani Belarus
Matokeo ya awali yamempa Lukashenko mwenye umri wa miaka 70 ushindi wa asilimia 86 ya kura. Kiongozi huyo amekuwa akiendesha operesheni kali ya ukandamizaji dhidi ya wapinzani tangu maandamano makubwa kufanyika dhidi yake mnamo mwaka wa 2020.