Putin: Mazungumzo na Marekani yanaleta matumaini
27 Februari 2025Matangazo
Putin ametoa matamshi hayo alipokuwa akizungumza na maafisa wa Idara ya Usalama wa Taifa , FSB, mjini Moscow.
Amesema mikutano miwili ya awali imetoa ishara kwamba pande zote mbili zinayo shauku ya kurejesha tena mahusiano. Wanadiplomasia wa Urusi na Marekani walikutana hii leo mjini Istanbul kujadiliana juu ya kumaliza mivutano na kurejesha hali ya kawaida hasa kwenye balozi za nchi hizo mbili.
Huo ni mkutano wa pili kati ya maafisa Marekani na Urusi ndani ya kipindi cha wiki mbili baada ya mkutano mwingine uliofanyika mjini Riyadh wiki iliyopita.
Rais Donald Trump wa Marekani anachukua hatua za kimarisha tena mahusiano yalipwaya kati ya nchi yake na Urusi tangu Moscow ilipoinyakua rasi ya Crimea kutoka Ukraine mwaka 2014.