Putin huenda akakutana na Trump wiki ijayo
8 Agosti 2025Matangazo
Naibu balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Dmitry Polyanskiy hata hivyo amesema hana taarifa kuhusu mkutano unaopangwa kati ya Putin na rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskiy.
Hakujafanyika mkutano wowote wa kilele kati ya viongozi wa Marekani na Urusi tangu Putin na rais wa zamani wa Marekani Joe Biden walipokutana mjini Geneva mnamo Juni mwaka 2021. Urusi iliivamia Ukraine Februari 2022 kwa kile ilichosema ni kitisho kwa usalama wake.
Ukraine na washirika wake nchi za Magharibi wanatilia shaka uvamizi huo wakiueleza kama unyakuzi wa mabavu wa ardhi wa mfumo wa kikoloni.