Putin hatohudhuria mazungumzo ya amani Istanbul
15 Mei 2025Matangazo
Putin ameyasema haya usiku wa kuamkia leo wakati alipokuwa akitangaza ujumbe utakaoiwakilisha Urusi katika mazungumzo hayo.
Putin amemtuma mshauri wake Vladimir Medinsky kuelekea Istanbul kama mkuu wa ujumbe wa Urusi. Ujumbe huo utamjumuisha pia naibu waziri wa ulinzi wa Urusi Alexander Fomin na naibu waziri wa mambo ya kigeni Mikhail Galuzin.
Zelenskiy amesema iwapo Putin hatowasili kwa mazungumzo hayo na ataendelea na kile alichokiita, michezo, basi hiyo itakuwa ishara ya mwisho kwamba hataki kuvimaliza vita hivyo.
Afisa mmoja mwandamizi wa Ukraine ambaye hakutaka kutajwa jina usiku wa kuamkia leo ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa Zelenskiy alikuwa njiani kuelekea Uturuki.