Putin aizuru Kursk, tangu Urusi iwaondoe wanajeshi
21 Mei 2025Matangazo
Kulingana na ikulu ya Kremlin, Putin alilizuru eneo hilo jana ambapo alifika katika kiwanda cha nyuklia cha Kursk na kuzungumza na baadhi ya wafanyakazi.
Haya yanafanyika wakati ambapo kombora la Urusi katika kituo cha kijeshi cha kufanyia mazoezi kaskazini mashariki mwa Ukraine limesababisha vifo vya wanajeshi 6 na kuwajeruhi wengine 10.
Eneo lililo mpakani la Sumy ambapo Urusi ilianzisha uvamizi wake wa Ukraine mwaka 2022, limekuwa likishambuliwa mara kwa mara katika miezi ya hivi karibuni.
Wakati huo huo, Waziri wa Ulinzi wa Ujerumani Boris Pistorius leo ametoa wito wa hatua zaidi kuchukuliwa ili kuzuia uwezo wa kifedha wa Urusi.
Pistorius ameyasema haya kufuatia hatua ya Umoja wa Ulaya kuiwekea vikwazo zaidi Urusi.