Putin ataka mazungumzo ya ana kwa ana na Ukraine
11 Mei 2025Akizungumza mapema Jumapili Putin amependekeza kuwa majadiliano hayo yafanyike mjini Istanbul nchini Uturuki Mei 15. Hata hivyo hakusema lolote kuhusu mapendekezo ya awali yaliyotolewa na washirika wa Ukraine ya kusitisha vita kwa siku 30 yanayoungwa mkono na Marekani.
Soma zaidi: Ukraine yasema iko tayari kwa usitishwaji wa muda wa mapigano
Ametaka majadiliano anayoyapendekeza yafanyike bila masharti yoyote na kuwa angezungumza na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan asaidie kuyawezesha. Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amesema ni ishara nzuri kuwa Urusi imeanza kufikiria kuvimaliza vita lakini hatua muhimu ya kufikia hatua hiyo ni kuanza kusimamisha mapigano Mei 12
Kwa upande wake Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameukosoa mpango huo wa Putin akisema usitishaji vita bila masharti hautanguliwi na mazungumzo, na kuwa Putin anatafuta njia ya kuchelewesha usitishaji wa vita.