Putin asifu juhudi za Marekani za kumaliza vita Ukraine
15 Agosti 2025Rais wa Urusi Vladimir Putin amesifu "juhudi za dhati" za Marekani za kutaka kumaliza vita nchini Ukraine kabla ya mkutano wa kilele na Rais Donald Trump.
Putin ametoa kauli hiyo wakati alipozungumza na mawaziri waandamizi na maafisa wa usalama wakati akijiandaa kukutana na Trump hii leo jimboni Alaska.Ni yepi matarajio ya Waukraine kutoka mkutano wa Trump na Putin?
Mkutano wa viongozi hao wawili unasubiriwa kwa shauku kubwa na ulimwengu na huenda ukatoa mwelekeo wa kukomeshwa kwa vita kubwa zaidi barani ulaya tangu vita ya pili ya dunia.
Rais Trump ameelezea matumaini yake kwamba Rais Putin yuko tayari kumaliza vita vyake Ukraine, lakini kuna uwezekano makubaliano yoyote ya amani yakahitaji mkutano mwingine utakaomshirikisha kiongozi wa Ukraine.Ukraine, Ulaya na Trump waungana kabla ya mkutano na Putin
Rais Volodmyr Zelensky na washirika wake wa Ulaya wameongeza juhudi mapema wiki hii za kuzuia makubaliano yoyote ambayo yataitenga Ukraine.