Putin asema yuko tayari kukutana na Zelensky
19 Juni 2025Licha ya nia yake ya kukutana na Zelensky, Putin alisisitiza masharti makali ya amani, ikiwa ni pamoja na madai ya Ukraine kukubali kupoteza maeneo zaidi na kuachana na ushirikiano na mataifa ya Magharibi, masharti ambayo maafisa wa Ukraine wameyataja kuwa matakwa yasiyokubalika.
Moscowinaendelea kukataa usitishaji mapigano usio na masharti na, kwa mujibu wa Kyiv, inatumia mazungumzo ya amani kama hila ya kuchelewesha kumalizika kwa vita.
Putin atoa onyo kwa Ujerumani
Putin pia alitoa onyo kali kwa Ujerumani, akisema kuwa utoaji wowote wa makombora ya Taurus kwa Ukraine utakuwa ishara ya ushiriki wa moja kwa moja wa Ujerumani katika vita hivyo.
Alithibitisha pia kuwa yuko tayari kuzungumza na Kansela Friedrich Merz, lakini alitupilia mbali uwezekani wa Berlin kuwa mpatanishi huru kutokana na msaada wake wa kijeshi kwa Kyiv.
Putin atilia shaka uhalali wa Zelensky
Katika hotuba yake, Putin alisema mkataba wowote wa amani lazima uwe na dhamira ya kuhakikisha uthabiti wa muda mrefu na kuzuia migogoro ya baadaye.
Hata hivyo, alitilia shaka uhalali wa Zelensky kwa kuhoji uhalali wa mamlaka yake chini ya sheria ya kijeshi.
Watu 28 wauawa Ukraine katika shambulizi kali la Urusi
Katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, waokoaji wametoa miili zaidi kutoka kwenye kifusi cha jengo la makazi lililoharibiwa na shambulizi kali zaidi la kombora la Urusi mwaka huu.
Russia, USA, zakubaliana kufikisha mwisho vita Ukraine
Shambulizi dhidi ya jengo lenye ghorofa tisa katika wilaya ya Solomianskyi limesababisha vifo vya watu 28.
Watu ishirini na watatu walifariki ndani ya jengo hilo lilipoanguka, na wengine watano walipoteza maisha maeneo mengine ya jiji hilo wakati Urusi ilipoanzisha mashambulizi makubwa ya anga kwa kutumia zaidi ya droni 440 na makombora 32.
Russia yaigusa pabaya Ukraine, Kyiv yajibu mapigo
Wahudumu wa dharura walitumia kreni na mbwa waliopokea mafunzo maalum kusaka manusura huku familia zikiwa zinasubiri kwa huzuni karibu na eneo hilo.
Serikali ya Ukraineilitangaza Jumatano kuwa ni siku ya maombolezo ya kitaifa, ambapo maua na mishumaa iliwekwa karibu na eneo la tukio.
Manusura walielezea usiku wa hofu, huku wengi wakijificha kwenye korido za majengo wakati droni zikiendelea kushambulia maeneo jirani.
Putin akanusha kulengwa kwa makazi ya raia
Putin amekanusha uharibifu kwa raia na kudai kuwa vikosi vya Urusi havilengi maeneo ya makazi, madai yanayopingwa na ushahidi mwingi unaotoka Kyiv na miji mingine.
Alieleza mashambulizi ya kijeshi ya Urusi kuwa ni jibu kwa upanuzi wa NATO, na kusisitiza kuwa Urusi ina faida ya kimkakati kwenye uwanja wa mapambano.
"Vikosi vyetu vinaendelea kusonga kila siku,” alisema, akipuuza hofu kuhusu kuongezeka kwa silaha za NATO.
Marekani yalaani shambulizi kali la Urusi dhidi ya Ukraine
Wakati juhudi za amani zinazoongozwa na Marekani zikiwa zimekwama, utawala wa Trump ulilaani shambulizi jipya la Urusi, ukilitaja kuwa ni ukiukaji wa mchakato wa amani.
Ubalozi wa Marekani mjini Kyiv ulisema kuwa shambulizi hilo linapingana na wito wa Rais Trump wa "kusitisha mauaji na kumaliza vita.”
Trump asema atakutana 'haraka sana' na Putin.
Hata hivyo, Ukraine imekosoa jumuiya ya kimataifa kwa kupoteza mwelekeo kutokana na migogoro mingine kama mvutano wa Mashariki ya Kati na mizozo ya kibiashara, huku Urusi ikiendeleza mashambulizi yake.