Putin: Tutaendelea kuimarisha uwezo wa kijeshi wa Urusi
23 Februari 2025Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema wanajeshi wake walioko nchini Ukraine wanatetea maslahi ya kitaifa na ameapa kuwa na dhamira isiyotetereka ya kuimarisha vikosi vya jeshi la nchi yake katika ulimwengu unaobadilika kwa haraka.
Putin ametoa matamshi hayo kuelekea kumbukumbu ya miaka mitatu ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, hatua iliyochochea mzozo mkubwa barani Ulaya tangu vita ya pili ya dunia.Urusi na Marekani zakubaliana kufanya mazungumzo bila ya Ukraine
Katika mkanda wa vidio uliochapishwa na Ikulu ya Kremlin katika siku ya maadhimisho ya watetezi wa taifa la Urusi, Putin ameongeza kuwa wataendelea kuboresha uwezo wa kijeshi, utayari wao wa mapigano kama sehemu muhimu ya usalama wa Moscow.
Ukraine ilivamiwa na Urusi mnamo Februari 24 mwaka 2022, huku Kremlin ikidai kuwa inajilinda dhidi ya kitisho cha NATO na kuzuia upanuzi wa taasisi hiyo.