Rais wa Urusi Vladimir Putin asema atawasaidia watu wa Iran
23 Juni 2025Urusi imetoa ahadi hiyo baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, kufanya ziara fupi nchini humo na kukutana kwa mazungumzo na Putin.
Ingawa haijawa wazi ni msaada wa aina gani Urusi itakaotoa kwa Iran, msemaji wa Ikulu ya Kremlin Dmitry Peskov amesema kitakachotolewa kitategemea na ombi la Jamhuri hiyo ya Kiislamu. Urusi, hata hivyo, ilipendekeza kujitolea kuwa mpatanishi wa mgogoro unaoendelea Mashariki ya Kati.
Marekani yashambulia vinu vitatu vya nyuklia nchini Iran
Iran imekuwa ikiipa silaha Moscow katika vita vyake vinavyoendelea na Ukraine na mataifa hayo mawili ni washirika wakubwa wa kimkakati.
Kando na mazungumzo yake na Abbas Araghchi, Rais Putin pia alizungumza na Waziri Mkuu wa Iraq Mohammed al-Sudani kuhusu mgogoro huo wa Mashariki ya Kati.