PUNJAB:Mukhataran Mai mwanamke aliyenajisiwa,Pakistan akata rufaa dhidi ya kuachiwa watuhumiwa
27 Juni 2005Matangazo
Mwanamke wa kipakistan aliyenajisiwa na watu waliodai kupewa amri hiyo na wazee wa kijiji amekata rufaa kwenye mahakama kuu dhidi ya kuachiliwa huru watuhumiwa wa kosa hilo.
Katika kisa kilichogonga vichwa vya habari kimataifa,Mukhataran Mai alinajisiwa mwaka 2002 katika mji wa Meerwala ulioko wilaya ya Punjab, kama adhabu kutokana na madai ya kakake kuhusiana kimapenzi na mwanamke kutoka ukoo mwengine.
Wanaume sita walihukumiwa kifo kuhusiana na kosa hilo lakini baadae mahaka iliwaachia huru watano kati yao na kumfunga mtuhumiwa wa sita kifungo cha maisha gerezani.
Mai anaitaka mahakama kuu kuwarudishia tena hukumu ya kifo wanaume hao waliohusika kumnajisi.