Polisi yazuia maandamano Tanzania
5 Januari 2008DAR-ES-SALAAM:
Polisi Tanzania,jirani ya Kenya,imepiga marufuku maandamano yaliopangwa hii leo na vyama vya upinzani
Kuonesha umoja na mshikamano na mtetezi wa wadhifa wa urais alieshindwa nchini Kenya Raila Odinga.
Akitoa kielezo kwanini upinzani nchini tanzania haukuruhusiwa kuandamana, afisa mkuu wa polisi Alfred Tibaigana alisema,
„Hali isio ya usalama nchini Kenya imezusha pia wasi wasi wa usalama nchini Tanzania. Kufanya maandamano kuungamkono upande mmoja wa mgogoro uliozuka kutachafua zaidi hali ya mambo.“
Mkuu huyo wa polisi alisema vyama 4 vikuu vya Upinzani nchini Tanzania-Civic United Front (CUF),Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) NCCR-Mageuzi na Tanzania Labour Party (TPL) vilitoa taarifa kwa polisi kuiarifu azma yao ya kuandamana hii leo mjini Dar-es-salaam.
Tibaigana alisema kwamba vyama hivyo 4 vya upinzani vimekataa kuvunja maandamano yao.Akasema polisi imewataka wakaazi wa jiji la Dar-es-salaam kuyasusia maandamano hayo yaliotishwa na upinzani.